JE EPL NI BORA KULIKO LALIGA?
Ebu leo twendeni taratibu kwa kuelewana kabisa. Ukiwasikiliza watu wengi wanaosema ligi bora na ngumu yenye mvuto duniani ni EPL... Huku wakisema La Liga ni ligi ya kibiashara zaidi... Swali linalokuja kama Epl ndio bora , mbona vilabu vyenye mafanikio ulaya vipo Spain ? Mbona wachezaji bora walioitikisa dunia wengi wamepita Spain ? Messi , Cristiano Ronaldo , Zidane , Kaka, Ronaldinho , Cryuff , seedorf, Robben, Neymar na etc.. Kwa nini Epl ni ligi bora halafu hawajapita bora katika bora ? Wanasema Epl ni kipimo cha ubora , mbona likija suala la mchezaji wao , wanasema ili uwe bora sio lazima upite Epl ? tushike kipi sasa ? Mbona tuzo kubwa duniani , wachezaji kutoka La Liga ndio wamezitawala kwa kiwango kikubwa ? Kwani Epl hakuna wachezaji bora , wakuweka challenge kwa wachezaji wa La Liga ? Mnasema Spain ina mvuto ndio maana wachezaji wao wanakuwa rahisi kubeba tuzo , Kwa hiyo ligi dhaifu chapa yake ni kubwa kuliko ligi bora , tunakubaliana hapo ? Unakuta mtu anasema Epl ...