JE EPL NI BORA KULIKO LALIGA?



 Ebu leo twendeni taratibu kwa kuelewana kabisa.

Ukiwasikiliza watu wengi wanaosema ligi bora na ngumu yenye mvuto duniani ni EPL...

Huku wakisema La Liga ni ligi ya kibiashara zaidi...

Swali linalokuja kama Epl ndio bora , mbona vilabu vyenye mafanikio ulaya vipo Spain ?

Mbona wachezaji bora walioitikisa dunia wengi wamepita Spain ?

Messi , Cristiano Ronaldo , Zidane , Kaka, Ronaldinho , Cryuff , seedorf, Robben, Neymar na etc..

Kwa nini Epl ni ligi bora halafu hawajapita bora katika bora ?

Wanasema Epl ni kipimo cha ubora , mbona likija suala la mchezaji wao , wanasema ili uwe bora sio lazima upite Epl ? tushike kipi sasa ?

Mbona tuzo kubwa duniani , wachezaji kutoka La Liga ndio wamezitawala kwa kiwango kikubwa ?

Kwani Epl hakuna wachezaji bora , wakuweka challenge kwa wachezaji wa La Liga ?

Mnasema Spain ina mvuto ndio maana wachezaji wao wanakuwa rahisi kubeba tuzo , 

Kwa hiyo ligi dhaifu chapa yake ni kubwa kuliko ligi bora , tunakubaliana hapo ?

Unakuta mtu anasema Epl ni bora halafu GOAT wake mpira wake wote kamalizia Spain kwenye ligi wanayosema sio bora tukuelewe vipi ?

Kwa nini Mfungaji bora namba 1 na 2 wa muda wote kwenye Uefa Champions league ni Malegend wa La Liga sio Epl ?

Mbona hawa wachezaji mnaosema wanacheza kwenye ligi bora Uingereza wakiulizwa timu za ndoto zao wanataja timu za Spain ?

Hivi kweli mchezaji anaweza kuichagua timu inayocheza kwenye ligi dhaifu ?

Kwa nini klabu zenye fan base kubwa duniani mbili za juu zote zinatoka Spain ambayo mnaiita ligi dhaifu (Madrid & Barca) halafu ndio inakuja united ?

Kwa nini klabu zenye Followers wengi ukijumlisha kwenye platforms zote ni klabu kutoka Spain ndio zimekuwa zikiongoza (Madrid & Barca) kisha ndio inakuja klabu za Epl ?

Kimahesabu nadharia zote zimekataa kuonesha ukubwa wa Epl badala yake zinaonesha thamani na ukubwa wa La Liga...

Nyie mnaosema EPL ni bora kuliko La Liga , ebu nielewesheni ndugu yenu nielewe...

Comments

Popular posts from this blog

LAMINE YAMAL NA LEONEL MESSI.

MANCHESTER UNITED IS ABOUT TO SELL KOBBIE MAINOO AFTER THE END OF THIS SEASON.

KNOW THE AFRICAN FOOTBALL.